Pin Song

Diamond Platnumz azidi kupanda daraja, Sasa kuwania BET Award kipengele cha Best International Act: Africa

Ilikua stori kubwa pale Diamond Platnumz alipotangazwa kushiriki kwenye tuzo za MTV Base (Mama Awards) kikiwa ni kituo kingine kikubwa cha burudani Afrika.
Leo hii Diamond Platnumz ameingia kwenye stori nyingine kubwa ya dunia baada ya kuchaguliwa kushiriki kwenye tuzo za Television kubwa ya Marekani ya BET ambapo yupo kwenye kipengele cha wanaogombea BEST INTERNATIONAL ACT AFRICA.
 Anaigombea hiyo tuzo na Davido wa Nigeria, Mafikizolo wa South Africa, Tiwa Savage wa Nigeria, Toofan na Sarkodie wa Ghana. the OFFICIAL nominees 2014!….

BET kupitia page yao ya twitter waliandika kuthibitisha kuchaguliwa kwa Diamond na kumpongeza akiwa pia ni msanii pekee wa Afrika Mashariki kwenye tuzo hizi za mwaka huu.

No comments