MTV MAMA 2014: Diamond hakubahatika, Mafikizolo wabeba tuzo kubwa zaidi, orodha kamili ya washindi

Safari ndefu ya ya mchakato wa tuzo za MTV (MAMA2014) Ulioanza rasmi
April 16 baada ya kutangazwa majina ya nominees na kuanza kupigiwa kura
imefikia ukingoni usiku wa kuamkia leo, ICC Arena, Durba Afrika
Kusini.  



Kwa mujibu ya matokeo ya mchakato mzima, Tanzania hatubahatika kupata
tuzo hata moja kati ya tuzo mbili alizokuwa anawania Diamond Platinumz
(Best Male Artist na Best Collaboration).  Davido ndiye aliyebeba tuzo
ya Best Male Artist na tuzo nyingine kubwa ya Artist of The Year. Na
Tiwa Savage aliipeleka Nigeria tuzo ya Best Female.



Kundi la Mafikizolo kutoka Afrika Kusini ndilo lililonyakua tuzo kubwa
zaidi usiku huo, tuzo ya Wimbo bora wa mwaka na wimbo wao maarufu wa
Khona waliomshirikisha Uhuru. Pia likashinda tuzo ya kundi bora (Best
Group).



Mafikizolo wanawania pia tuzo za BET katika kipengele cha Best
International Act.  Moja kati ya surprise zilizowavuta wengi ni pale
D’Banj alipoungana na Trey Songz jukwaani.



Macho ya watanzania na nguvu kubwa inaelekezwa BET ambako Diamond anawania tuzo ana kila dalili ya kuwazidi wenzake.

Hii ni orodha ya washindi:                                                                                        

Song of The Year
Khona-Mafikizolo feat Uhuru


Best Collabo
Y-tjukutja – Uhuru feat DJ Buckz, Oskido, Professor, Yuri Da Cunha


Best Music Video
Clarence Peters (Nigeria)


Best Francophone
Toofan (Togo)


Artist of the Year
Davido (Skelewu)


Best Hip Hop
Sarkodie (Ghana)


Best Group
Mafikizolo


Best New Act
Stanley Enow (Cameroon)


Best Female Artist
Tiwa Savage (Nigeria)


Best Male Artist
Davido (Nigeria)


Best Altenative
Gangs of Ballet  (South Africa)
*Transform Today Award- Clarence Peters


ad

2 thoughts on “MTV MAMA 2014: Diamond hakubahatika, Mafikizolo wabeba tuzo kubwa zaidi, orodha kamili ya washindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *