Pin Song

New AUDIO | Mzungu Kichaa ft Juma Nature - Together As One | Download

Mzungu Kichaa atoa single yake ya pili kutoka kwenye CD yake mpya iitwayo RELAX. Katika wimbo huu amemshirikisha Juma Nature na Karen Mukupa. Mzungu Kichaa alikuwa na haya ya kusema, "Juma Nature ndiye aliyenipa jina langu la kisanii nilivyokuwa nikifanya featuring kwenye nyimbo kadhaa za Bongo Flava mwaka 1999 na 2000. Pia niliweka vocals pamoja na TID kwenye wimbo wa Nature uitwao Hili Game. Kwahiyo nina furaha kubwa kupata fursa ya kufanya kazi na Juma Nature tena katika wimbo hii. Karen Mukupa pia alishawahi kushirikiana na Nature siku za nyuma na ni rafiki yetu sote wa siku nyingi. Karen ni msanii mkubwa sana nchini Denmark anapotokea na nimefurahi kuweza kuwashirikisha wote wawili." Mzungu Kichaa pia alisema kuwa wimbo huu ni kwaajili ya kujenga umoja ili kufikia malengo na ndoto katika fani ya muziki. Wimbo huu unazungumza kwa niaba ya wasanii wote wa Afrika Mashariki.


Vocals zimerekodiwa studio ya MJ Records na ngoma zimerekodiwa live ndani ya Caravan Records na Abdalla Membe, Shabani Rashid (keyboard), Kevin Mpangala (Bass), Mzungu Kichaa (Guitar).
http://bit.ly/togetherAsOne

No comments