Ujio mpya wa Nikki Mbishi, One The Incredible & Songa Feat. Lady Jay Dee – Kupanda na Kushuka

Wakitokea Tamaduni Music; Nikki Mbishi akiwa na One
The Incredible
pamoja na Songa wamemshirikisha Lady Jaydee katika kazi
yao mpya Kupanda Na Kushukawanayotarajia kuiachia hivi karibuni.
Akiongelea kuhusu wimbo huo, Mbishi ameelezea sababu ya kuwashirikisha
One Incredible, Songa pamoja na Jide kuwa ni kutaka kutengeneza muziki
mzuri kwani wote kwenye wimbo huo wana ladha adimu hivyo wote kuwa
katika kazi moja kutafanya wimbo uwe bora zaidi hivyo fans wategemee
kitu kizuri kutoka kwao…


“Unajua muziki sometimes unahitaji vitu fulani ili uwe mzuri zaidi na
hii ni kawaida ya muziki ulivyo. Kwahiyo tukaona tukifanya kitu kwa
pamoja kitakuwa safi, tukaingia studio za Man Walter tukafanya wimbo ‘Kupanda na Kushuka‘.
Ni wimbo ambao unaelezea maisha ya kawaida , kupanda na kushuka kwa
maisha, leo umepata kesho  umelala njaa lakini ni maisha….”

ad

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *