Ali Kiba afunguka kuhusu bifu na Diamond

Hatimaye staa wa Bongofleva Ali Kiba amekiri kuwa yuko katika
bifu na mwanamuziki mwenzie Diamond Platnumz kwa zaidi ya miaka mitatu
sasa.

Kauli hiyo ya Ali Kiba inapingana na ile ya hivi
karibuni iliyowahi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati za bunge ya Hesabu
za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisisitiza kuwa wanamuziki hao hawana
tofauti zozote na kwamba ni watu tu ndio wanakuza suala hilo.

Hata hivyo, juzi Ali Kiba aliliambia gazeti Moja[Mwananchi]
kuwa ni kweli kuna ugomvi baina yao, huku akisisitiza kwamba tofauti yao
ilianza mwaka 2012. Wakati Ali Kiba akifunguka kuhusu bifu hilo hali
imekuwa tofauti kwa Diamond ambapo amekaririwa mara kadhaa kuwa hana
tofauti yeyote na mwanamuzi huyo ambaye wanatoka mkoa mmoja wa Kigoma na
kuunganisha Kundi la Kigoma All Stars. Akizungumza wakati akijibu
maswali mbalimbali katika mahojiano maalumu, mwanamuziki huyo pia
alielezea mambo mengi kuhusu muziki wake na hii ni sehemu ya mahojiano
hayo;

Swali: Nini chanzo cha bifu lako na Diamond?

Ali Kiba: Hakuna kiini kwa sababu nadhani hayo
mimi aaah.…Kiukweli haya tuliyamalizaga muda mrefu …Labda watu wahisi
kwamba kipindi kile alichonifuta katika wimbo wake (alisema bila
kufafanua jina la wimbo) na yeye alivyosema kwamba nimemfuta katika
wimbo wangu ‘Single Boy’, mimi sijawahi kurekodi na Diamond katika wimbo
wangu hata mmoja na huo niliimba na Lady Jaydee.

Yeye ndiye aliyesema kwamba nilimfuta katika wimbo
ule, ila ukweli ni kwamba hatukuwahi kuingia pamoja studio, nilimshauri
tufanye wimbo mwingine lakini siyo ule kwa sababu nimeshaimba na Lady
Jay Dee.

Swali: Umeshawahi kuwa karibu na Diamond?

Ali Kiba: Hapana yeye ndiyo alishawahi kuwa na ukaribu na mimi.

Swali: Unaweza kufanya kolabo na Diamond?

Ali Kiba: Ngoja nikwambie ukweli, sidhani kama
ninaweza kuja kufanya kolabo na Diamond, ila nikipata wimbo ambao
nadhani kwamba anastahili kuwapo, kiukweli nitamshirikisha lakini kama
hastahili haitawezekana.

Kwa sababu kila wimbo unajielezea, kwa mfano kama
mtu anataka kufanya Zouk akimtafuta Stara Thomas itawezekana kwani hayo
ndiyo mambo yake, kwa hiyo kama nikitaka kufanya naye wimbo ambao
nitaona kwamba unafaa nitamfuata na nitamweleza.


Swali: Utofauti kati yako na Diamond ni upi? 

Ali Kiba: Mimi naimba muziki mzuri na nina ‘hit song’, naye
Diamond anaimba ‘hit song’, unaposema mimi sina hit song wakati mimi
nina nyimbo nyingi kushinda yeye unakuwa unakosea, tangu nimeanza kuimba
ni nyimbo mbili tu hazijawahi kuwa hit ikiwamo ‘My Everything’ na ‘Mali
Yangu’ lakini nyingine zote zilivuma tangu nianze kufanya muziki.

Swali: Inasemekana katika Tamasha la
TigoMusic kuna hirizi zilionekana Uwanja wa Leaders na wewe na Diamond
mnatuhumiwa kuhusika, unalizungumziaje?

Ali Kiba: Yaani Mungu mmoja sina imani hiyo kabisa
na mimi naamini Mungu na mambo ya hirizi na mimi ni tofauti. Nadhani
watu wanasema hivyo kwa sababu wanadhani kwamba kuna bifu. Binafsi sina
bifu na msanii yeyote labda kama wanaweza kuwa na bifu na mimi binafsi
simchukii msanii yeyote na sina bifu na yeyote.

Swali: Video yako ya Mwana imezungumziwa
na mashabiki kuwa haikuwa na uhalisia. Pia ilikuwa ya kawaida sana, wewe
binafsi unalichukuliaje?

Ali Kiba: Video ilivyokuwa ndivyo ilipangwa iwe
kwa sababu kila mtu alikuwa amejenga picha itakuwaje kwa hiyo
ililazimika kufanya vile kwa kuwa watu walishapanga mpaka gharama kwa
kuwa nilikaa muda mrefu pasipo kufanya. Ningefanya kitu ambacho watu
walikifikiria kiukweli ingekuwa karaha, nilichozingatia mimi ni kuimba
vizuri na kuonyesha fikra za wimbo husika.

Swali: Vipi uliandaa ‘skripti’ ya video au aliamua GodFather kuifanya vile ilivyotengenezwa?

Ali Kiba: Tulikuwa na ‘script’ yetu pia waongozaji wa
video walikuwa na yao ambayo walitupatia. Hivyo tukakubaliana nao kwa
sababu tulitaka kuleta utofauti na kila kitu kikakaa sawa.

Swali: Ni kweli kwamba una mpango wa kufanya kolabo na Chris Brown?

Ali Kiba: Uwezekano wa kufanya upo kwa sababu kila
kitu ni mipango kwa hiyo naweza kufanya kolabo na wasanii wa kimataifa
na mashabiki watarajie kufanya hivyo.

Swali: Kwa nini haujafanya video ya
Kimasomaso na ulisema video ya Mwana ingefanyika Dar es Salaam kwa nini
ulitengenezea Afrika Kusini?

Ali Kiba: Video ya ‘Kimasomaso’ ilishindikana
kutokana na muda ulikuwa hautoshi, nilijikuta niko katika mambo mengi
sana kwani nilikuwa nimeegemea katika video ya Mwana kwa hiyo nilipokuja
kugeuka ikawa ni vigumu.

Nilisema kwamba nyingine ningefanya nje ya hapa
lakini kwa ‘Mwana’ sijaelewa kwanini nifanye hapa, tofauti na hiyo
nyimbo haikuwa na maana ya Dar es Salaam, maana yake ni mwanamke na
mwanamume sikuona sababu ya kufanyia hapa jijini.

Ukitumia neno la Dar es Salaam ni kwa sababu ni jiji lenye changamoto
kwa hiyo unapozungumzia hilo ina maana kwamba ni Joharnesburg, Nairobi,
Kampala, London majiji ambayo yana changamoto mfano video ya Macmuga
nilifanyia Marekani.




Twitter: @djmwanga     
Instagram: @djmwanga     
Facebook Fans Page: DJMwanga

ad

One thought on “Ali Kiba afunguka kuhusu bifu na Diamond

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *