Kalamu ya Nick wa Pili: Hip hop inavyoikwamisha Hip hop Tanzania

Hip hop kwa upande wa kwanza ni CNN,BBC ama TBC (Sauti) ya mageto na
mitaa mara nyingi ya watu wa chini. Na sehemu ya pili ni fursa ya
kuwatoa vijana magetoni na familia zao pia. Mfano akina Jay Z, Luda,
Eminem, Kanye, hawaishi tena kitaa ni matajiri wakubwa.

Hip hop Tanzania katika upande wa sauti ya mtaa imefanya kazi kubwa
sana, toka nyimbo kama Dei Waka, Mikononi mwa polisi, Ndio Mzee, Chemsha
Bongo, Good Boy, Show Love, Niaje ni Vipi, Alikufa kwa Ngoma
nakadhalika. Kwakweli hamna jambo la kijamii ambalo hiphop haijaligusa,
kuna maktaba ya kutosha itakayosomwa vizazi na vizazi kwa maAna muziki
haufi.

Lakini katika upande wa kuwa fursa ya kuwatoa vijana bado haijafanya kazi kubwa kwanini?

Haswa kipindi hiki ambacho biashara ya muziki inakuwa kubwa Afrika na
bila shaka afro beat ndio muziki namba moja Afrika.Kuna mawazo miongoni
mwa wana hiphop ambayo yanachanganya na kupoteza mwelekeo wake, kwa
ambao hawata yatafakari.

Mawazo hayo ni kuwa hiphop ndio muziki wa kitaa lakini, ukiwa kitaani,
bodaboda, bajaji,saloon,klabu, masherehe kadhalika unaskia sana muziki
ya kuimba moto, Vanessa,Barnaba, chache za rap. Sasa hicho kitaa
tunachomanisha ni kipi? Wakuimba wao hawaishi kwa imani wanapushi muziki
yao kote kwenye harusi,mabaa,mageto, magari, vipindi vya asubuhi mpaka
usiku kote wamo.

Hip hop sio muziki wa media, lakini ndio wanaongoza kuwashambulia na
kuwalalamikia watu wa media na kuwatukana kwenye nyimbo? Kivipi sasa na
hiphop sio muziki wa media? Wakuimba wako bize kutafuta connection za
media ndani na nje ya nchi.

Sisi ni hiphop wale sio, wale laini hawakazi, commercial lakini! Hip hop
si ni uhalisia wa mawazo ya mhusika, experience yake ya maisha
aliyopitia, sasa unawezaje kujudge experience ya mtu na ukasema sio ya
kweli(not real) wakati wewe haujaipitia. Ni upotezaji focus, lini
umeskia afro beat wanasema sisi ndio wale sio?

Ushindani wa kushambuliana utaskia, madogo wameteka gemu wakongwe
wanahanya. Wakuimba wanashindana videos, colabo za kimataifa, mavazi
nakadhalika vitu vinavyoongeza thamani ya muziki.

Hip hop sio muziki wa biashara kweli? 2pac kauza kopi zaidi ya milioni
75, movies, mavazi kama rocawear, G-unit, labale kubwa kama Rock nation
vyote hivyo vimefanyika kupitia hip hop. Jay Z, ana zaidi ya dolla
milioni 800, Dre sasa ni billionaire. Waimbaji wanaongea biashara na
kujaribu vitu vikubwa, hip hop ina fursa kubwa lakini haya mawazo
yatakwamisha wengi.

Waimbaji wana bifu zisizo na madhara wanagombania mara wasichana ama
mambo ya kiki na zinawapa media platform na kuwakuza, hiphop matusi tena
mabaya, kutishiana mpaka kushambuliana na kuumizana, nakadhalika, ni
kuiangusha!

Anapotokea mwana hip hop anayetaka kujaribu muziki wake kufikia watu
wengi na kuwa na matumizi mengi yaani club, ghetto, kwenye mabar,
vipindi vyote, harusi, watu wa kwanza kumvuta shati watakuwa wana
hiphop! Utaskia ‘hakazi tena yule, ile laini’ badala ya kumwona kama mtu
anayetanua wigo,soko na kuongeza fan base na kufanya watu wengi kuwa
karibu na hip-hop

Kuzuia ubunifu wa kistyle, biti, melodi, ushairi. Katika hii dunia
inayokwenda kwa speed kali angalia matoleo ya simu yote ni kupata wateja
wengi, kuboresha huduma na kufanya isichoshe watumiaji. Angalia afro
beat wanavyobadili. Akina Wizkid, P-Square, Diamond, leo wamepiga dansi
hii kesho hii, mpaka wanaruka na parachute kwa video. Hip hop kivipi
ibaki vilevile? Generation zinabadilika, dunia inabadilika J-Cole hawezi
kuwa Nas wala 2 Pac.

Je kusipokuwa na mifano ya wana hip hop waliofanikiwa, mzazi gani
ataruhusu mwanae afanye hip hop na huo si ndio mwanzo wa kukosa vipaji
vipya!

Makala hii nimeandika kwaajili ya wadogo zangu wenye kipaji huko form
one. Msiwe kama sisi kuweni tofauti. Harakati ni pana Staki Kazi
itakwambia ujiajiri, Diamond, Joh Makini, Vanessa watakuonesha kwa
vitendo namna ya kujiajiri na wote hapo ni wana harakati kwa kuonesha
jamii njia.

Mfuate Nick wa Pili kwenye Twitter na Instagram kwa jina  @nikkwapili




Twitter: @djmwanga     
Instagram: @djmwanga     
Facebook Fans Page: DJMwanga

ad

One thought on “Kalamu ya Nick wa Pili: Hip hop inavyoikwamisha Hip hop Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *