Pin Song

New Music From Otuck. Video and Audio (Deja Vu Ft. Hance Puff)

 OTUCK: "Utabibu unanisaidia kufanya muziki mzuri"Muziki mzuri hutengenezwa kwa ustadi wa mchanganyiko wa ala za sauti na mashairi. Sanaa ya utengenezaji muziki mzuri ni kazi ambayo watayarishaji na wasanii kwa pamoja huifanya wakati wa utengenezaji wa wimbo. Mara nyingi, wasanii na watayarishaji wa muziki hutengeneza muziki kutokana na mazingira halisi yanayowazunguka katika maisha yao binafsi kama vile maisha ya mapenzi, kazi nk.
Otuck William, msanii mpya kwenye maskio ya wapenzi wengi wa muziki nchini ambaye pia ni Afisa Tabibu, anaelezea namna ambavyo kazi yake ya utabibu imechangia katika utengenezaji wake wa muziki.

"Siku yangu ya kawaida kwa kiasi kikubwa naitumia kusikiliza wagonjwa na wateja wengine wanaokuja kwenye kituo cha afya ninachofanyia kazi. Ni kitu ambacho ninakipenda maana kinanipa nafasi ya kusaidia jamii. Imekuwa ni ndoto yangu kwa muda mrefu. Lakini pamoja na kusikiliza matatizo yao ya afya, ukiwa mhudumu wa afya, watu hukuamini, wengi watakueleza matatizo yao ya ndani sana ambayo pengine hawawezi kuwaambia hata wapenzi wao, hivyo kuongea nao kila siku kunanipa nafasi ya kujifunza mengi sana kuhusu watu na Maisha. Muziki ninaoufanya ni kwa ajili ya watu na Maisha, hivyo yale nijifunzayo kwa watu niwaonao kila siku, huwa ninajaribu kuyatafsi katika ala za muziki. Ni namna moja wapo ya kutengeneza kitu ambacho kinawahusu watu moja kwa moja. Hivyo kinakuwa bora na kizuri..." - Otuck William

Pamoja na kazi nyingi ambazo ziko studio, mwimbaji huyu wa Soul anafanya vizuri kwenye vituo mbali mbali vya TV na Redio kupitia rekodi yake iitwayo "Deja Vu" ambayo imetayarishwa na yeye mwenyewe na video imeongozwa na kutayarishwa na Nikki Dizzo wa Focus Film Tanzania.

Kama bado hujapata nafasi ya kuangalia Video hiyo, hii hapa   

Lakini pia unaweza kupakua audio ya deja vu kwenye mtandao wa soundcloud.

https://soundcloud.com/otuckwilliam/deja-vu-otuck-william-ft-hance-puff

2 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Great Song From Doctor Of Music! Safi sana... Thumbs Up!!!

    ReplyDelete