Pin Song

MTV Base yatangaza kuanza kuicheza video ya Lupela yake Alikiba

Mashabiki wa Alikiba wamelala usingizi mnono baada ya kupewa habari njema waliyokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu. Video ya Lupela itaanza kuchezwa leo kwenye kituo cha runinga cha MTV Base.

Kiba alitangaza habari hiyo njema kwenye Instagram Jumanne hii.

“I can’t wait ..Thank You @mtvbaseafrica #KingKiba,” aliandika kwenye picha inayoonesha ratiba ya kuchezwa video hiyo iliyotoka wiki kadhaa zilizopita.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mashabiki wa Alikiba kuanza kumshambulia meneja wake, Seven Mosha kwenye Instagram kutokana na hadi sasa video hiyo kutooneshwa kwenye vituo vya kimataifa.

Haya ni baadhi ya malalamiko yao:

eng.allysm: @sevenmosha madam mbona mnatuangusha kwa Kiba mbona mambo ayaendi km tulivyo Taraji please unaweza nipa sababu kwanini nyimbo za Kiba azipigwi ktk TV za nje mf MTV na trace hasa lupela

alikiba_page: Video za alikiba azionyeshwi MTV na vtuo vingne vya kimataifa why this happen ….inafika kipind tunachoka management yake bhna ahaa
tamu_iwe_kavu: Ukweli usiopingika @sevenmosha mnamuangusha sana @officialalikiba.. Hatuzioni ngoma zake zikipigwa katika stesheni kubwa.. Hatuoni collabo za njee na wasanii wakubwa.. Mpo slow sana.. Sioni unavyompigania kiba kama unavyompigania jide.. Mnampotezea muda tu kiba…. Mnaboa kusema ukweli..

masco_the_don_master: Oya kama kazi imewashinda mwachen kiba tutamsimamia wenyewe coz haiwezekan lupela tokea imetoka haijapigwa trace,mtv na vituo vingine vya kimataifa wakati now asilimia 70 ya nyimbo za bongo mpaka za underground zinapigwa y kiba hapigwi???halafu kwa nn collabo hazionekan? Halafu mmnachelewa xana kutoa nyimbo y kila nyimbo baada ya miez 8??achen izo bhana mnamuua kiba halafu sisi ndio tunaopata tabu mtaani so kama kaz hamuwez achen

Download DJMwanga Android Application Click HERE
https://goo.gl/Dpx8j4
JIUNGE NAMI KUPITIA 
Twitter: @djmwanga     
Instagram: @djmwanga     
Facebook Fans Page: DJMwanga

No comments